Exodus 24

Agano Lathibitishwa

1 aKisha Mungu akamwambia Musa, “Njooni huku juu kwa Bwana, wewe na Haruni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli. Mniabudu kwa mbali, 2 blakini Musa peke yake ndiye atakayemkaribia Bwana; wengine wasije karibu. Nao watu wasije wakapanda pamoja naye.”

3 cMusa alipokwenda na kuwaambia watu maneno yote na sheria zote za Bwana, wakaitikia kwa sauti moja, “Kila kitu alichosema Bwana tutakifanya.” 4 dNdipo Musa akaandika kila kitu Bwana alichokuwa amesema.

Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.
5 eKisha akawatuma vijana wanaume wa Kiisraeli, nao wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu za mafahali wachanga kuwa sadaka za amani kwa Bwana. 6 fMusa akachukua nusu ya damu ya wale wanyama na kuiweka kwenye mabakuli na nusu nyingine akainyunyiza juu ya madhabahu. 7 gKisha akachukua kile Kitabu cha Agano na kuwasomea watu. Nao wakajibu, “Tutafanya kila kitu alichosema Bwana, nasi tutatii.”

8 hNdipo Musa akachukua ile damu, akawanyunyizia wale watu, akasema, “Hii ni damu ya agano ambalo Bwana amelifanya nanyi kufuatana na maneno haya yote.”

9Musa na Haruni, Nadabu na Abihu, pamoja na wazee sabini wa Israeli wakapanda mlimani, 10 inao wakamwona Mungu wa Israeli. Chini ya miguu yake kulikuwa na kitu kama sakafu ya mawe ya yakuti samawi, iliyo safi kama anga angavu. 11 jLakini Mungu hakuinua mkono wake dhidi ya hawa viongozi wa Waisraeli; walimwona Mungu, nao wakala na kunywa.

12 k Bwana akamwambia Musa, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.”

13 lBasi Musa akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Musa akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. 14 mMusa akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Haruni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”

15 nMusa alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, 16 onao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Musa kutoka katikati ya lile wingu. 17 pKwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima. 18 qKisha Musa akaingia ndani ya lile wingu alivyokuwa akipanda mlimani. Naye akakaa huko mlimani kwa muda wa siku arobaini, usiku na mchana.
Copyright information for SwhKC